Jumanne, Februari 28, 2017

WAKATI WAKITESWA NA NJAA, 117 WAFA KWA MAFURIKO ZIMBABWE

Shirika la ulinzi wa kiraia la Zimbabwe limesema watu wasiopungua 117 wamefariki kutokana na mvua kubwa inayonyesha katika miezi ya hivi karibuni, na wengine 106 wamejeruhiwa baada ya kupigwa na radi.
Nyumba zaidi ya 1,930 zimeharibiwa na familia 635 zimekosa makazi. Mvua hiyo pia imeathiri shule, hospitali, barabara na kubomoa baadhi ya madaraja.
Zimbabwe imekuwa inakumbwa na mvua kubwa kuanzia mwezi Januari, ambayo imejaza mabwawa ya maji na kuleta tishio la mafuriko.
Mbali na mvua Zimbabwe, wiki iliyopita Zimbabwe ilikumbwa na kimbunga cha Dineo kilicholeta uharibifu kwenye maeneo mengi, hasa kwa eneo lililoko chini la Tsholotsho, kaskazini magharibi mwa Zimbabwe, na kufanya watu wasiopungua 850 kupoteza makazi.

0 comments:

Chapisha Maoni