Wanasayansi wameonya kuwa wakulima wadogo wa kanda ya Afrika Mashariki wanaweza kukabiliwa na tatizo la uhaba wa chakula kutokana na mashamba yao kuvamiwa na viwavijeshi.
Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Kuboresha Mahindi na Ngano cha Mpango wa Mahindi Duniani CIMMYT, Bw Prasanna Boddupalli amesema wadudu hao wameharibu takriban eka laki 2.87 za mahindi tangu mwaka jana.
Amefafanua kuwa utafiti uliofanywa mwaka jana kwenye mashamba ya wakulima umethibitisha kuwa wadudu hao wanasambaa haraka nchini Kenya na Uganda, na kusababisha hatari kubwa katika nchi hizo zinazokabiliwa na ukame.
Ameyataka mashirika ya kitaifa ya utafiti katika nchi hizo kuanzisha mfumo madhubuti wa usimamizi wa wadudu, ikiwemo kutoa onyo mapema kwa wakulima kupambana kwa ufanisi na uvamizi wa viwavijeshi.
0 comments:
Chapisha Maoni