Jumanne, Februari 28, 2017

MIJI SABA YA TANZANIA KUNUFAIKA NA MKOPO WA BENKI YA DUNIA

Benki ya dunia (World Bank) imeidhinisha mkopo wa dola milioni 130 kwa mradi wa kuendeleza miundombinu katika miji saba nchini Tanzania.
Benki hiyo imesema kuwa wenyeji wa miji hiyo sita; Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Dodoma, Mbeya na Mtwara watapata huduma bora zaidi mradi huo utakapokamilika. “Uboreshaji wa miundombinu katika miji inayoendelea nchini Tanzania ni muhimu katika kuafikia lengo la kuendeleza viwanda nchini,” Bella Bird, mkurugenzi wa World Bank nchini Tanzania alisema.
Mradi huo kwa jina “Tanzania Strategic Cities Project” (TSCP) ulianzishwa mwaka wa 2010. Mradi huo wenye gharama ya dola milioni 175.5 unafadhiliwa na World Bank kwa dola milioni 163 huku serikali ya Denmark ikichanga dola milioni 12.5 iliyosalia.

0 comments:

Chapisha Maoni