Jumatatu, Februari 13, 2017

TAARIFA NYINGINE YA WATANZANIA 8 WALIOKAMATWA MALAWI

Mashirika ya haki za binadamu ya Tanzania yameonyesha wasiwasi kuhusu walichoita unyanyasaji dhidi ya watanzania waliokamatwa kwa tuhuma za kuingia kwenye maeneo wasiyotakiwa na kufanya ujasusi.
Watanzania nane walikamatwa mwezi Desemba mwaka jana kwenye mpaka kati ya Tanzania na Malawi katika wilaya ya mpakani ya Karonga baada ya kujaribu kuingia kwenye mgodi wa madini ya Uranium, na baadaye kupelekwa mahakamani.
Uchunguzi uliofanywa na taasisi mbili za kutetea haki za binadamu za Tanzania umeonyesha kuwa haki za kimsingi za watu hao, ikiwa ni pamoja na mawasiliano na wanasheria wao na familia zao na kununua chakula kwa kutumia pesa zao zinazuiwa.
Vyomba vya habari vya Malawi vinasema watu hao ni majasusi waliotumwa na serikali ya Tanzania kwenye kuchunguza kama Malawi inatengeneza silaha za nyuklia, na walikuwa na vifaa vya kutia shaka.

0 comments:

Chapisha Maoni