Jumanne, Februari 28, 2017

RAIS MPYA WA SOMALIA ATANGAZA JANGA LA NJAA NCHINI HUMO

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo hapo jana (Jumanne) alitangaza ''janga la kitaifa'' kutokana na ukame mkali ambao umewaathiri watu milioni tatu.
Rais Farmajo ameiomba jumuiya ya kimataifa kushughulikia haraka mzozo huo ili kuepusha maafa ya kibinaadamu.
Shirika la Afya Duniani, WHO mapema wiki hii lilionya kuwa Somalia iko katika hatari ya kukumbwa na njaa kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha miaka 25.
Njaa ya mwaka 2011 iliwaua kiasi ya watu 260,000.

0 comments:

Chapisha Maoni