Jumatatu, Februari 13, 2017

POLISI MKOANI MBEYA WATOA ORODHA YA WAFANYA BIASHARA NA WATUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA +AUDIO

Kufuatia mapambano yanayoendelea nchi nzima dhidi ya watu wanaojihusisha na uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanya misako na Mafanikio yaliyopatikana katika Misako ni kama ifuatavyo:-


Mnamo tarehe 11.02.2017 majira ya saa 02:00 usiku, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilifanya misako katika maeneo ya Manga na Nsalaga – Uyole na kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na wauzaji, wasambazaji na watumiaji [mateja]. Watuhumiwa waliokamatwa kutokana na kujihusisha ba usambazaji na uuzaji wa dawa za kulevya ambao ni 1. SHABAN RAMADHAN [40] Mkazi wa Uyole 2. RASHID YASIN [35] Mkazi wa Nonde 3. RODA MWAMBERA [60] Mkazi wa Mama John 4. MRISHO RAMADHAN [22] Mkazi wa Airport - Iyela na 5. MUSSA KIMBE [33] Mkazi wa Nonde. 
Watuhumiwa wote wapo mahabusu na mahojiano zaidi yanaendelea ili kubaini mtandao mzima wa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya. 
Aidha kufuatia misako iliyofanyika kuanzia tarehe 19.01.2017 hadi tarehe 09.02.2017 katika maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya, Watuhumiwa wawili walikamatwa katika matukio mawili tofauti wakiwa na dawa za kulevya. 
Katika msako wa kwanza uliofanyika maeneo ya Ilemi Jijini Mbeya, HENRY MWAMFUPE [19] Mkodishaji Baiskeli na Mkazi wa Ilemi alikamatwa akiwa na kete 03 za dawa za kulevya aina ya Heroine. 
Pia katika msako uliofanyika maeneo ya Mbalizi, ANITHA ABEL [21] Mwanafunzi wa Kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Sanani iliyopo Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe na Mkazi wa Mbalizi alikamatwa akiwa na kete 15 za dawa za kulevya aina ya Heroine akiwa nyumbani kwao. 
Mtuhumiwa anaishi na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la MARTHA MWALINDU ambaye alikimbia baada ya kuwaona askari na inasadikika ndiye muuzaji/msambazaji mkubwa wa dawa hizo za kulevya na huwa anamtumia mtoto wake kuuza na kusambaza. Msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa zinaendelea. 
Watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya Upelelezi kukamilika. 
Aidha katika misako mbalimbali iliyofanyika walikamatwa watuhumiwa wanaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya maarufu kama Mateja ambao ni:- 

1. AYUBU ABDALLAH [42] Mkazi wa Ilomba jijini Mbeya 

2. EMANUEL SIMBEI [43] Mkazi wa Sokomatola 

3. IMAN ABBAS [33] Mkazi wa Majengo 

4. SHABAN SHAIBU [19] Mkazi wa Nonde 

5. KENY SANGA Mkazi wa Sokomatola 

6. PASCHAL PIUS [28] Mkazi wa Itiji 

7. PILIM KAYANGE [20] Mkazi wa Uhindini 

8. ELISHA MWAIHABI [19] Mkazi wa Nonde 

Wengine ni:- 

9. DANIEL KANJANJA [43] Mkazi wa Uhindini 

10. MUSSA KIPESA [37] Mkazi wa Iwambi 

11. CHARLES GERVAS [28] Mkazi wa Nonde 

12. KIMANZI KILONZA [44] Mama John 

13. SHABAN SHAIBU [26] Mkazi wa Nonde 

14. EMANUEL LUCAS [18] Mkazi wa Ilomba 

15. RICHARD GONDWE [40] Mkazi wa Ivumwe 

16. HENRY LEMA [35] Mkazi wa Mama John 

17. RAMADHAN ABBAS [18] Mkazi wa Sae 

18. EDWARD MWASEKA [30] Mkazi wa Majengo 

19. LUSEKELO KIDION [26] Mkazi wa Mwakibete 

20. ALINANUSWE STIVEN [26] Mkazi wa Ilolo 

21. JUSTIN WISTON [23] Mkazi wa Mafiati 

22. MICHAEL KASHILILIKA [20] Mkazi wa Manga 

23. KANI ASANGALWISYE [28] Mkazi wa Ituha. 

Watuhumiwa wapo mahabusu wanaendelea kuhojiwa ili kupata mtandao halisi wa wauzaji na wasambazaji wa dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua watu na mtandao wa watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. 
Aidha Kamanda KIDAVASHARI anatoa wito kwa wananchi kufanya kazi na kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani inasababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Hapa ni wakati RPC Kidavashari akitoa orodha hiyo;

0 comments:

Chapisha Maoni