Mtu mwengine aliyeteuliwa na rais wa
Marekani Donald Trump, kujaza wadhfa wa waziri wa jeshi la wanamaji
amejiondoa baada ya kuonekana kukiuka sheria za taifa kuhusu mgongano wa
maslahi.
Philip Bilden ameeleza wasiwasi wake kuhusu maisha yake
ya usiri na changamoto alizokumbana nazo katika kujitenganisha na
biashara zake.
Waziri wa usalama, Jim Mattis, amesema atampendekeza mtu atakayechukua nafasi ya Bilden katika kipindi cha siku chache zijazo.
Mteuliwa wa Rais Trump aliyependekezwa kusimamia jeshi la Marekani alijiondoa mapema mwezi huu.
0 comments:
Chapisha Maoni