Zulia jekundu limetandikwa katika ukumbi wa Dolby uliopo jijini Los Angeles kwa ajili ya sherehe za mwaka huu za Oscars.
Maandalizi
ya mwaka huu yamekuwa magumu kutokana na changamoto kadhaa ikiwemo
maandamano, na hali mbaya ya hewa mbaya ambayo haikutarajiwa iliyopiga
eneo la California, hata hivyo hakuna mvua inayotarajiwa pindi wasanii
nyota watakapoanza kuwasili.
Tuzo kuu inatabiriwa kwenda kwa Picha
bora ya mwaka , filamu ya muziki ya La La Land,wakati huo huo,
mwigizaji nyota Denzel Washington ndiye anayeongoza katika
kinyang'anyiro cha mwigizaji bora.
Denzel Washington , ni miongoni
mwa nyota wa kiafrika wanagombe kushinda tuzo yenye umbo la sanamu ya
dhahabu baada ya kutowakilishwa kwa miaka miwili, jambo ambalo liliibua
kampeni iliyopewa jina la Oscar ni ya watu weupe.
0 comments:
Chapisha Maoni