Bingwa wa ndondi uzani Welterweight duniani Manny Pacquiao, atapigana na Muingereza Amir Khan tarehe 23 mwezi Aprili,
Pigano
hilo litaandaliwa baada ya mashabiki wa Pacquaiao kwenye mtandao wa
Twitter kumchagua Khan kama mwanandondi ambaye wangependa apigane na
mfilipino huyo.
"Hiki ndicho mashabiki walikuwa wanaaka," Pacquaiao mwenye umri wa miaka 38 alisema.
Khana
wa umri wa miaka 30 alithibitisha pigano hilo licha ya Pacquaiao kusema
kuwa huenda pigano lake likaandaliwa Milki ya nchi za kiarabu, eneo
litakaloandaliwa bado halijatangazwa.
Akiongea kwa njia ya video Khan anasema Uingereza, Dubai au Marekani ni kati sehemu ambapo pambano hilo litafanyika.
Pigano
la mwisho la Khan lilifanyika mwezi Mei mwaka 2016, wakati wakati
alimshinda kwa Knock out raia wa Mexico Saul "Canelo" Alvarez.
0 comments:
Chapisha Maoni