Maonyesha ya kulitambulisha vazi la stara na staha
ya mwanamke wa Kiislamu Hijabu pamoja na thamani nyingine za Kiislamu
yamefanyika katika jimbo la California nchini Marekani.
Maonyesho hayo yamefanyika kwa
juhudi za wanachuo wa Kiislamu wa Chuo Kikuu cha Chapman cha California
na lengo hasa la maonyesho hayo ni kukabiliana na taswira isiyo sahihi
kuhusiana na Uislamu na hisia za chuki dhidi ya dini hiyo tukufu.
Kwenye maeonyesho hayo ya Hijabu kulionyeshwa pia nakala ya tarjuma ya Kiingereza ya Qur'ani Tukufu.
Katika hali ambayo serikali ya Rais
Donald Trump wa Marekani inatekeleza siasa za kuwabana Waislamu, wafuasi
wa dini hiyo nchini Marekani katika majuma ya hivi karibuni wameandaa
ratiba na shughuli mbalimbali za kuitambulisha dini Tukufu ya Kiislamu
katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Aidha ratiba na shughuli kama hizo za
kuutambulisha Uislamu, zimekuwa zikifanyika pia katika nchi kadhaa za
Ulaya ikiwemo Uingereza.
Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa,
Uislamu ndiyo dini inayokuwa kwa kasi zaidi barani Ulaya na kwamba,
licha ya propaganda chafu za vyombo vya habari vya Magharibi, idadi ya
watu wanaosilimu na kuingia katika dini tukufu ya Kiislamu imekuwa
ikiongezeka kila siku, suala linaloonyesha kufeli njama na propaganda
chafu dhidi ya Uislamu na Waislamu.
0 comments:
Chapisha Maoni