Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe umeikumba wilaya ya Kalambo mkoa wa Rukwa kusini magharibi mwa Tanzania, na kusababisha vifo vya nguruwe karibu 200.
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Bibi Julieth Binyura amesema serikali imepiga marufuku biashara ya nyama hiyo, na usafirishaji wa nguruwe hai ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo. Bibi Binyura pia amesema wanavijiji wa wilaya hiyo wamearifiwa kuhusu ugonjwa huo. Ofisa mifugo wa Wilaya hiyo Bw Wilbrod Kansapa amesema nguruwe wanaoonekana wakirandaranda wanakamatwa.
Ufugaji wa nguruwe unaendelea kuongezeka katika maeneo ya magharibi mwa Tanzania, kutokana na mahitaji makubwa kwenye miji mikubwa kama Dar es salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni