Jumanne, Februari 14, 2017

AISHITAKI KAMPUNI YA TAXI BAADA YA KUBAINI ILIMPELEKA MKEWE KWA MCHEPUKO

Mfanyibiashara mmoja kusini mwa Ufaransa ameshtaki kampuni ya Texi ya 'Uber', baada ya mkewe kufahamu kwamba safari zake alizofanya na magari hayo zilikua za kumtembelea mpenzi wake.

Mwanamme huyo aliitisha huduma ya Uber akitumia simu ya mkewe na hata baada ya kufunga akaunti hiyo , upande wa Uber haukufunga bali uliendelea kutuma jumbe kwa simu ya mkewe kuhusu safari yake na hii ilimfanya mke wake kumshuku.
Wawili hao wametalakiana kutokana na kisa hicho na mwanaume huyo anataka uber imlipe faini ya dola milioni 48.
Gazeti Le Figaro limenadi kwamba kumekua na matatizo ya simu za Uber ambapo ukisha funga kaunti yako baada ya kutumia mtandao wake, kampuni hiyo haifungi akaunti hiyo. 
Uber haijatoa taarifa yeyote kuhusu kisa hiki ila imesema inatilia maanani sana masuala binafsi ya wateja wake.

CREDIT: LE FIGARO

0 comments:

Chapisha Maoni