Jumanne, Januari 17, 2017

NABII AAMURU WAUMINI KUNYWA KEMIKALI ZA INJINI ILI KUPONA

Mtu mmoja anayejiita nabii nchini Afrika Kusini amesababisha wafuasi wake kunywa kemikali ya kusafisha injini, akidai kuwa ina uwezo wa kuponya na ina ladha ya asali.
Theo Bongani Maseko wa kanisa la Breath of Christ Ministries, anasema kuwa kemikali hiyo hushambulia virusi kwenye mwili wa binadamu, na kutambua mashetani.
Mtu huyo ni kati ya wanaume kadha ambao wamezua shutuma kwa kuwamwagia watu dawa ya kuuaa wadudu na pia kuwashauria kula wanyama.
Bwana Maseko alinukuliwa akisema kuwa kemikali hiyo haina athari za kiafya.
"Ina ladha ya asali , nimekunywa mara mbili."
Aliongeza kuwa watu watatu wameponywa kwa kunywa kemikali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni