Jumanne, Januari 17, 2017

MAFUA YA NDEGE YAZUIA MIFUGO RWANDA

Waziri wa kilimo wa Rwanda Geraldine Mukeshimana ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa za mifugo kutoka Uganda na nchi za Ulaya kuacha kuagiza kwa muda bidhaa zote za mifugo kutoka Uganda na nchi za Ulaya kutokana na mlipuko wa homa ya mafua ya ndege katika maeneo hayo.
Waziri huyo amewataka wafugaji wote kufungia mifugo yao ili kuepuka mwingiliano kati yao na ndege wasiofugwa, na kwamba watu wanatakiwa kukaa mbali na ndege pori ambao watakutwa wamekufa, na kutoa taarifa haraka kwa mamlaka husika.
Uganda imethibitisha kuwa mlipuko wa ugonjwa huo unaambukiza kwa ndege, ambao pia unaweza kuwapata binadamu. Wizara ya kilimo ya Uganda imesema ndege waliopatwa na ugonjwa huo mpaka sasa ni ndege aina ya Membe, bata na kuku.

0 comments:

Chapisha Maoni