Mwananchi – Tanzania
Mbarali kwafurika watu wa kushuhudia kupatwa kwa jua
Maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wasomi na wanafunzi wamefika katika mji mdogo wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya kwa lengo la kushuhudia tukio la kihistoria la kupatwa kwa jua kuanzia saa 4.15 asubuhi leo hadi saa 7.59 mchana.
Mwananchi – Tanzania
Msigwa athibitishwa mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu
Rais John Magufuli amemthibitisha Gerson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais Ikulu. Msigwa amethibitishwa kuanzia Agosti 31 kushika wadhifa huo.
The Standard – Kenya
CORD kuteua mgombea wa urais mwezi Januari mwakani
Muungano wa upinzani wa CORD utachagua mgombea urais katika mkutano wa wajumbe utakaofanyika Januari mwakani. Mpaka wakati huo, viongozi wa CORD Raila Odinga, Kalonzo Musyoka, na Moses Wetang’ula wanatakiwa kuvijenga zaidi vyama vyao.
The Standard – Kenya
Kitendo cha kuhama chama chawachanganya wabunge wa Jubilee
Naibu rais wa Kenya William Ruto amewaambia wabunge wa muungano wa Jubilee kuwa uongozi wa muungano huo umedhamiria kuzuia wabunge kuhama kabla ya kura inayotarajiwa kupigwa leo. Akizungumzia jambo hilo, Ruto amewataka wabunge wanaodhamiria kutoka kwenye muungano huo kuondoka mapema kuliko kuvuruga ilani ya chama cha Jubilee, ambayo itazinduliwa wiki ijayo.
Daily Monitor – Uganda
Besigye kuhutubia mkutano wa kisiasa Marekani
Kiongozi wa upinzani Dr. Kizza Besigye anatarajiwa kuhutubia mkutano wa mwaka wa jamii ya Waganda wanaoishi Amerika Kaskazini, katika juhudi zake za kuwafahamisha Waganda waishio nchi za nje hali ya kisiasa ilivyo nchini humo.
Daily Monitor – Uganda
Viongozi wa mabaraza ya vyuo vikuu watakiwa kuacha mgomo
Prof Mauda Kamatenesi, amewataka viongozi wa mabaraza ya vyuo vikuu nchini Uganda kuacha kuchochea mgomo kama njia ya kuwasilisha matatizo ya wanafunzi na badala yake, kujitahidi kutafuta suluhisho kwa njia ya amani.
Habari Leo – Tanzania
CHADEMA wakubali yaishe
Wakati leo wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa wamejipanga kufanya mikutano na maandamano nchi nzima, Kamati Kuu ya chama hicho imetangaza kusitisha kampeni hiyo iliyopewa jina la Ukuta.
Habari Leo – Tanzania
Ongezeko la VAT halijaathiri mapato ya utalii
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe amesema wizara yake imejiwekea mkazo mkubwa kuhakikisha mchango wa utalii katika Pato la Taifa unafikia asilimia 20 kutoka asilimia 17.5 ya mwaka jana.
The New Times – Rwanda
Rwanda, Benin zaunga mkono mkuu wa Benki ya Dunia kuendelea na wadhifa wake
Rwanda na Benin zimeeleza kuunga mkono kuchaguliwa tena kwa mkuu wa sasa wa Benki ya Dunia Dr Jim Yong Kim, na kusema kiongozi huyo ana uwezo mkubwa na nia halisi ya maendeleo.
The New Times – Rwanda
Ushirikiano katika usalama ni muhimu, asema Kagame
Rais Paul Kagame ametoa wito kwa wakuu wa polisi katika kanda ya Afrika Mashariki kuimarisha ushirikiano wao katika kukabiliana na uhalifu, hususan uhalifu unaoibuka sasa ikiwa ni matokeo ya maendeleo ya hivi karibuni ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
0 comments:
Chapisha Maoni