Jumapili, Septemba 04, 2016

UNAAMBIWA ZAIDI YA TANI 7,000 ZA TAKATAKA ZINAIZUNGUKA DUNIA KATIKA ANGA YA JUU KWA KASI YA KILOMETA 10 KWA SAA 1

Wanasayansi wa NASA wamekadiria kuwa takataka zaidi ya laki 5 zenye uzito wa zaidi ya tani 7,000 zinazunguka dunia yetu katika anga ya juu kwa mwendo kasi wa kilomita 10 kwa sekunde. Mwendo kasi huo ni mkubwa kuliko risasi, hivyo satilaiti na vyombo vingine vya anga hata vikigongwa na takataka yenye ukubwa wa hata kama mchanga tu, vitakumbwa na ajali.
Takataka za anga ya juu ni pamoja na mabaki ya roketi, vyombo vya anga visivyotumiwa tena, na vyombo vya anga vilivyovunjika, si kama tu ni tishio kwa vyombo vya anga vinavyotumiwa, bali pia huenda vitatishia usalama wa viumbe duniani.
Mwaka 2009 satilaiti za Marekani na Russia ziligongana, na kusababisha takataka 2000 kubwa na takataka nyingine nyingi ndogondogo kubaki katika anga ya juu.
Kampuni ya Rand ya Marekani iliwahi kutoa ripoti kuhusu suala hili, ikisema ingawa pande mbalimbali zimetambua hatari ya takataka hizi, lakini inaonekana kwamba hazitatenga fedha na kutafuta utatuzi wa makini hadi ajali kubwa itokee.
NASA imeunga mkono baadhi ya miradi midogo ya utafiti wa takataka za anga ya juu, lakini bado haijachukua hatua yoyote ya kutatua kihalisi tatizo hili. Mchambuzi mmoja wa mambo ya safari ya anga ya juu na ulinzi alisema hakuna idara maalum inayoshughulikia suala hili, kwani hili ni gumu sana.

0 comments:

Chapisha Maoni