Zaidi ya watu laki 3 wanatarajiwa kuhudhuria maonyesho ya kilimo ya Kenya jijini Mombasa yanayofunguliwa tarehe 30.
Afisa mkuu mtendaji wa maonyesho hayo Batram Muthoka amesema maonyesho ya mwaka huu yatafunguliwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta tarehe 1 Septemba.
Akizungumza na wanahabari,Bw Muthoka pamoja na mwenyekiti wa Pwani wa maonyesho ya kilimo Brown Ondego wamehimiza wakulima kuhudhuria maonyesho ya mwaka huu wakisema kutakuwa na mafunzo mengi mapya ya kilimo.
Mwaka jana maonyesho ya Mombasa yaalihudhuriwa na zaidi ya watu 250,000 na ongezeko la watu mwaka huu litafungua fursa zaidi za biashara.
Maonyesho ya mwaka huu yanajiri wakati ambapo maelfu ya wakaazi wa pwani katika sehemu za Ganze na Bamba wanakumbwa na baa la njaa.
Wizara ya kilimo Kenya imehimiza wakaazi wa maeneo kame aidha kujiingiza kwenye kilimo cha unyunyizaji.
0 comments:
Chapisha Maoni