Jumatatu, Mei 16, 2016

UNAFAHAMU NINI KUHUSU MAGONJWA YA MOYO? UNAJUA KUWA HUJA GHAFLA? NI NINI USIFANYE NA NINI UFANYE?


Duniani kila siku kuna watu wanaokufa ghafla kutokana na ugonjwa wa moyo, japo watu wengi wanaonekana kama ni wazima sana, lakini ugonjwa wa moyo ni wa ghafla na ni wa dharura, wengi hawajui kama wamepata ugonjwa huo hadi itokee ajali, kwani kujikinga na kifo hicho tunatakiwa kuwa na tahadhari mapema na watafiti wanatushauri mambo yafuatayo ambayo hutakiwi kuyafanya mara kwa mara:
Kwanza, usipitie barabara yenye kelele nyingi mara kwa mara, kwani kelele zinazotokana na magari, pikipiki n.k zinausumbua ubongo wa watu, na pia uchafuzi wa hewa unazidisha uwezekano huo, hasa kwa watu waliopanda baiskeli, kwani wanavumilia mazingira mabaya huku wakitumia nguvu ya kuendesha baiskeli, inawezekana kusababisha ukosefu wa Oxygen na kuwa na mzunguko mbaya wa damu mwilini.
Pili, usitumie nguvu kubwa kwa ghafla wakati unapojisaidia, kitendo hicho cha kutumia nguvu kubwa kwa ghafla kinasababisha kirahisi kupanda kwa shinikizo la damu na pia kwa moyo, ambapo inaweza kusababisha kupasuka kwa mishipa ya damu
Tatu, usinywe pombe na kahawa kupita kiasi, ambazo zote zinaharakisha mwenendo wa moyo, mtu mzima mwanaume anashauriwa asinywe pombe zaidi ya 750ml kwa ujumla kila siku na kwa mtu mzima mwanamke anashauriwa asinywe zaidi ya ml 450 kila siku. Na watu wenye ugonjwa wa moyo pia wanashauriwa wasinywe kahawa na pombe kwa afya yako.
Nne ni kuvuta sigara au kutumia dawa za kulevya, kama tujuavyo kwa wale wanaotumia cocaine, hatari ya kupata ugonjwa wa moyo ni mara 23 kuliko wale ambao hawafanyi hivyo.
Tano ni kutumia chumvi au sukari kupita kiasi, kula chumvi nyingi kunasababisha mishipa ya damu kuwa migumu na kupasuka kirahisi.
Sita ni kutokuwa na furaha kila siku, yaani kuwa na hasira siku zote zinazoambatana na wasiwasi kunasababisha kupoteza usingizi, hivyo moyo wako hauwezi kupata mapumziko ya kutosha na kupandisha shinikizo la damu na kiwango cha udonda wa moyo. Unashauriwa kuzungumza na marafiki na familia yako ukipata shida kubwa.
Saba ni kukaa kwa muda mrefu bila kufanya mazoezi yoyote. Kwani itaharibu mzunguko wa damu na kukwama damu ndani ya sehemu fulani mwilini.

0 comments:

Chapisha Maoni