Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeiamuru Kampuni ya Ndege ya
Fastjet kumlipa abiria wake, John Mhozya fidia ya Sh30 milioni baada ya
kushindwa kumtaarifu kuhusu kuahirishwa kwa safari yake.
Mbali na
fidia hiyo ya hasara ya jumla aliyoipata abiria huyo kutokana na safari
hiyo kufutwa, pia Mahakama hiyo imeiamuru kampuni hiyo kumrejeshea
abiria huyo nauli yake ya Sh43,000 alizokuwa ameshalipa na Sh339,000
alizozitumia kwa nauli baada ya kutafuta usafiri mbadala kutoka shirika jingine la ndege.
0 comments:
Chapisha Maoni