Alhamisi, Aprili 07, 2016

WATU 11,595 WALIOKUWA WAMETEKWA NA BOKO HARAM WOKOLEWA

Jeshi la Nigeria limeokoa takriban watu 11,595 waliokuwa wameshikwa mateka na kundi la wanamgambo wa Boko Haram katika kipindi cha mwezi moja uliopita.
Kulingana na taarifa uliotolewa na jeshi kupitia msemaji wake Sani Usman, watu hao waliokolewa kwenye operesheni zilizofanywa kaskazini mashariki mwa nchi kati ya mwezi Februari 26 na Mechi 31 huku wengine wakikombolewa na maafisa wa usalama wa Cameroon.
Boko Haram wameua maelfu ya watu tangu kundi hilo lilipoanza mashambulizi kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka wa 2009. Ingawa jeshi la Nigeria limekomboa maeneo mbali mbali yaliyokuwa chini ya udhibiti wa Boko Haram, kundi hilo lingali lina uwezo wa kutekeleza mashambulizi hatari nchini humo.

0 comments:

Chapisha Maoni