Alhamisi, Aprili 07, 2016

NYUNDO NYINGINE KWA WATAALAMU KUTOKA NJE WANAOFANYA KAZI NCHINI TANZANIA

Serikali imepiga marufuku wataalamu kutoka nje ya nchi wanaokuja kufanya kazi za upimaji, upangaji na umilikishaji ardhi na kuagiza kuanzia sasa shughuli zote zitafanywa na kampuni za ndani ili kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zikitumika katika shughuli hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali inasema kwa sasa iko katika utekelezaji wa mpango wa kupima, kupanga na umilikishaji wa ardhi mpango amabo unatarajia kutekelezwa ndani ya miaka kumi huku ukitarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi tirioni 2.3.
Kauli hiyo ya serikali imekuja wakati wa uzinduzi wa bodi ya waalamu wa mipango miji na vijiji iliyoko chini ya uenyekiti wa Prof. Wilibad Kombe ambapo wamesisitizwa kuhakikisha wanatumia taaluma zao kumfanya kila mtanzania awe na umiliki wa ardhi tofauti na ilivyo hivi sasa.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake.
Pamoja na masuala mengine ameitaka bodi hiyo mpya kuhakikisha inashugulikia changamoto ya uhaba wa rasilimali watu.

0 comments:

Chapisha Maoni