Alhamisi, Aprili 07, 2016

SASA NI MARUFUKU KULIPIA NGONO UFARANSA

Wabunge nchini Ufaransa wamepitisha mswada ambao unaharamisha watu kulipa ili kupata huduma ya ngono na kuweka faini ya hadi dola 4,274 kwa wale watakaopatikana na hatia.
Wale watakaopatikana na hatia pia watalazimika kupewa mafunzo ya mazingira yanayowakabili makahaba.Imechukua zaidi ya miaka miaka miwili kupitisha mswada huo wenye utata kutokana na tofauti zilizopo kati ya mabunge mawili kuhusu swala hilo.
Baadhi ya makahaba waliipinga sheria hiyo wakati wa mjadala wa mwisho.
Waandamanaji 60 walipiga kambi nje ya bunge mjini Paris, walibeba mabango moja likiwa na maandishi yaliosema:''Sina haja ya kukombolewa, nitajikomboa mwenyewe'',kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Muungano wa makahaba wa Strass umesema kuwa hatua hiyo itaathiri maisha ya kawaida ya makahaba wanaodaiwa kuwa kati ya 30,000 na 40,000.
Lakini wanaounga mkono sheria hiyo wanasema itasaidia kukabiliana na mitandao ya ulanguzi wa binaadamu.
Pia itakuwa rahisi kwa makahaba wa kigeni kupata kibali cha kufanyia kazi kwa mda nchini Ufaransa iwapo watakubali kutafuta kazi zisizo za ukahaba.
Umuhimu wa sheria hiyo ni kushirikiana na makahaba ,kuwapatia vibali vya utambuzi kwa sababu tunajua asilimia 85 ya makahaba ni waathiriwa wa ulanguzi wa binaadamu ,mbunge wa chama cha kisosholisti Maud Oliver ambaye alifadhili sheria hiyo aliambia chombo cha habari cha AP.

0 comments:

Chapisha Maoni