Alhamisi, Aprili 07, 2016

BAJETI ILIYOTANGAZWA KATIKA MAKADIRIO YA FEDHA YA MWAKA 2016/2017

Serikali ya Tanzania jana (Jumatano) ilitangaza bajeti ya dola bilioni 13 katika makadirio yake ya fedha ya mwaka 2016/2017 itakayoanza mwezi wa Julai.
Bajeti hiyo inanuia kupunguza kwa kikubwa utegemezi wa wafadhili, alisema waziri wa fedha Philip Mpango huku akiongeza kuwa wafadhili watagharimia dola bilioni 1.5 pekee ya bajeti hiyo. Mpango alisema kuwa miradi nyingi ya maendeleo nchini humo imesimama kwa sababu ya wafadhili kutotoa ama kuchelewa kutoa fedha walizoahidi. “Serikali inafanya mazungumzo na wafadhili ili kuweka taratibu za kuaminika na kuhakikisha kuwa wafadhili wanatimiza ahadi wanazotoa,” Mpango aliambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam.
Waziri huyo alisema kuwa serikali ya Tanzania sasa inajitahidi kujitegemea kwa njia ya ukusanyaji wa ushuru ili kuepukana na masharti yanayotolewa na wafadhili. “Tunawaonya vikali wafanyibiashara wanaokwepa kulipa ushuru na wafanyikazi wa umma wanaotumia vibaya pesa za umma kuwa tutawachukulia hatua ya kisheria,” alionya waziri Mpango.
Katika hotuba yake bungeni mwezi Februari mwaka jana, Mpango aliambia wabunge kuwa serikali inanuia kupunguza utegemezi wa wafadhili kutoka asilimia 6.4 hadi asilimia tatu. Aliongeza kuwa upungufu huo utajazwa kwa kuongeza kodi inayotozwa juu ya mapato na asilimia 15 na kupunguza matumizi mabaya ya pesa za umma.

0 comments:

Chapisha Maoni