Jumapili, Aprili 03, 2016

WANAJESHI WA TANZANIA KUCHUNGUZWA JUU YA KASHFA ZA NGONO

Serikali ya Tanzania imesema kuwa itachunguza madai mapya ya unyanyasaji wa ngono dhidi ya wanajeshi wake wanaolinda amani nchini DRC (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).
Hii ni baada ya ujumbe wa walinda amani wa umoja wa mataifa nchini DRC kupokea malalamishi dhidi ya kikosi cha wanajeshi wa Tanzania chini yake. Ujumbe huo umesema kuwa unachunguza malalamishi ya unyanyasaji wa ngono dhidi ya wanajeshi wa Tanzania wanaohudumu katika kijiji cha Mavivi.

0 comments:

Chapisha Maoni