Mamia ya watu jana walijumuika pamoja jijini Nairobi katika hafla iliyojawa na majonzi kuadhimisha mwaka moja tangu shambulio la kigaidi katika chuo kikuu cha Garissa.
Chuo cha Garissa kilivamiwa na wanamgambo wa Al Shabaab tarehe mbili mwezi Aprili mwaka jana.
Takriban watu 148, wengi wakiwa wanafunzi, waliuawa na wengine 79 wakajeruhiwa kwenye shambulio hilo ambalo lilihuzunisha watu kutoka pembe zote za dunia. Wanamgambo hao walishika mateka wanafunzi 700 katika shambulio hilo na kuwatenga kwa msingi ya dini na kisha wakawafyatulia risasi wale ambao hawakuwa wafuasi wa dini ya kiislamu.
0 comments:
Chapisha Maoni