Ijumaa, Machi 04, 2016

WATU SABA WAFA MAJI ZIWA VICTORIA HUKO MWANZA, TANZANIA

Hapa nchini Tanzania, watu saba wa familia moja wamekufa maji na wengine wanne kunusurika baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kupinduka na kuzama Ziwa Victoria katika Mkoa wa Mwanza.
Familia hiyo ya watu 11 ilikuwa ikisafiri kutoka Kijiji cha Lubili wilayani Misungwi kwenda kwenye kikao mkoani Geita.
Mmoja wa walionusurika kwenye ajali hiyo, Juma Maguta alisema ajali hiyo ilitokea baada ya mtumbwi huo kupigwa na dhoruba.

0 comments:

Chapisha Maoni