Rubi ni aina moja ya kito adimu kitwacho Corundum. Corundum inatokana na atomu za Aluminum na Oxygen, kwa kawaida kito hiki ni angavu, lakini wakati kinapokuwa na madini kidogo ya chromium, kinaonesha rangi nyekundu na huitwa rubi, wakati kinapokuwa na madini ya titanium na chuma, kinaonesha rangi ya kibuluu na huitwa johari, na madini ya titanium na chuma aina ya ferric zitakifanya kuwa na rangi ya machungwa.
Silicon na chuma ni madini yanayopatikana kila mahali duniani. Hata johari na Corundum ya rangi ya machungwa zina madini kidogo ya chuma, ni jambo la ajabu kwamba rubi haina madini ya chuma.
Wataalamu wa jiografia wanasema, maeneo ambayo rubi inapatikana kimsingi yako katika ukanda wa marumaru ulioko kusini mwa Milima ya Himalaya. Ukanda huu wenye urefu wa kilomita elfu 3 unaanzia Tajikstan, kupitia Afghanistan, Pakistan, Kashmir, Nepal hadi China na Vietnam. Bamba la India liligongana na bamba la Eurasia na kuunga milima ya Himalaya, na kutengeneza rubi kutokana na mabadiliko ya kijiografia.
Nahitaji.kujifunz.aina.zamadini.nadhamizake
JibuFuta