Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema hawezi kugawana madaraka na kambi ya upinzani kwani alishinda kihalali kwenye uchaguzi mkuu wa Februari 18.
Akizungumza na kiongozi wa chama cha upinzani cha Farmers Party of Uganda (FPU), Meja Jenerali Benon Biraaro, Rais Museveni amesema anakaribisha pendekezo la kufanya mazungumzo na wapinzani kwa ajili ya kujadili mustakabali wa kisiasa wa taifa lakini hawezi kuunda serikali ya umoja wa kitaifa itakayowashirikisha wanasiasa wa upinzani.
Amesema uchaguzi ulikuwa fursa nzuri kwa wanasiasa kujitafutia vyeo na kama wapinzani walishindwa kuwashawishi wapiga kura, wanapaswa kusubiri hadi uchaguzi ujao na wala si kutumia njia za mkato kuingia serikalini.
Huku hayo yakijiri kuna tetesi kwamba kiongozi wa upinznai, Kizza Besigye ametoweka na hajulikani aliko. Duru za habari zinasema Besigye ambaye alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani hayuko tena nyumbani kwake. Polisi ya Uganda imekataa kuthibitisha au kukanusha suala hilo.
0 comments:
Chapisha Maoni