Watafiti wa Marekani wamegundua kuwa kemikali ya kuhifadhi ya aina ya Paraben inatiwa katika mafuta ya kujipaka mwilini lakini ingawa idadi ya kemikali hiyo ni ndogo, inaweza kuongeza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Watafiti wa chuo kikuu cha California wamesema, kiwango cha kusababisha saratani cha kemikali hiyo kimezidi matokeo ya utafiti wa awali, na kutoa mashaka kuhusu upimaji wa usalama ulikadiria pungufu la athari ya kemikali hiyo.
Kemikali ya Panraben inatumiwa katika mafuta ya kujipaka mwilini kama vile shampuu, mafuta ya kujikinga na miale ya jua, ambayo utafiti wa awali ulithibitisha kuwa kugusa kwa kupita kiasi kemilika hiyo kutaongeza hatari ya kupata saratani ya matiti na maradhi ya uke. Hivyo watafiti wanaona matumizi ya mafuta hayo yanaweza kuleta hatari kwa mwili wa binadamu.
0 comments:
Chapisha Maoni