Jumatatu, Machi 28, 2016

WATU 500,000 NCHINI KENYA HAWAJUI KUWA WANAISHI NA HIV

Utafiti nchini Kenya unaonyesha kuwa watu 500,000 hawafahamu kwamba wana virusi vya HIV.
Utafiti huo kwa jina Assisted Partner Notification Services unaonyesha kuwa kwa kila watu watatu walio na HIV mtu wa nne hupata kutambuliwa kutokana na habari zinazotolewa na mtu waliyeshiriki naye ngono.
Dr. Peter Cherutich kutoka wizara ya Afya nchini humo ambaye aliongoza utafifi huo amesema kwa kuwatumia watu ambao tayari wameambukizwa HIV wanaweza kuwafuatilia wapenzi wao na kuanza kutoa ushauri na matibabu kwao mara moja ili kuzua ueneaji na athari zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni