Mashirika matatu ya kikanda ya Afrika, COMESA, EAC na SADC, leo yamezindua mradi wa pamoja wa umeme ambao utaunganisha Zambia, Tanzania na Kenya.
Mtaalamu wa nishati wa COMESA Bw. Seif Elnasr Mohamedain amesema, mashirika hayo yanaharakisha utekelezaji wa mradi huo na kuhakikisha fedha za ujenzi wa mradi huo zinapatikana.
Bw. Seif ameongeza kuwa, Umoja wa Ulaya umetoa Euro milioni 4.4 kwa ajili ya mradi huo.
Awamu ya kwanza cha mradi huo inatarajiwa kumalizika Desemba mwaka huu.
0 comments:
Chapisha Maoni