Jumatatu, Machi 21, 2016

WAPENDA SOKA WATATU WAUAWA UWANJANI MOROCCO

Mashabiki watatu wa soka waliuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika mapigano yaliyozuka kati ya mashabiki wa timu Raja Casablanca huko Morocco, polisi alisema siku ya Jumapili.
Video ambazo zimeenea katika mtandao zilionyesha matokeo ya vurugu ya kutisha kati ya mashabiki wa Raja Casablanca mwishoni mwa mechi katika uwanja wa Mohammed V stadium huko Casablanca.
Mashabiki wawili waliaga dunia papo hapo,lakini kijana mwenye umri wa miaka 14 aliaga siku ya jumapili kutokana na majeraha aliyoyapata,maafisa wa usalama walisema.
Watu Arobaini na moja walikamatwa kwa kushiriki katika mapigano hayo na vitendo vya uharibifu nje ya uwanja, polisi alisema, akibainisha kwamba uchunguzi ilifunguliwa kuamua hali ya vurugu na kukamata wale wote waliohusika.

0 comments:

Chapisha Maoni