Wakaazi wa kijiji cha Mutakura, mjini Bujumbura wamegundua kaburi la siri lenye miili tano wiki tatu tu baada ya kupatikana kwa kaburi lingine la halaiki mjini humo.
“Wananchi walitujulisha kuhusu kaburi lililokuwa katika eneo la Mutakura likiwa na miili 5 ambayo inaaminika kuwa ya watu waliounga Rais Nkurunziza kuwania awamu ya tatu katika uchaguzi uliopita,” Eddy Hakizimana, msimamizi wa kitongoji cha Ntahangwa alisema. Alisema kuwa tayari maafisa wa serikali wamefukua mwili mmoja na wanaendelea kufukua miili mingine iliyobaki ili kuitambua.
Mnamo Februari 29, kaburi la halaiki lenye miili 30 liligunduliwa katika kijiji cha Mutakura ambacho kilikuwa ngome kuu ya maandamano dhidi ya Rais Nkurunzinza kuwania muhula wa tatu. Zaidi ya watu 400 wanaaminika kuuawa kwenye maandamano hayo huku wengine 240,000 wakikimbilia mataifa mengine.
0 comments:
Chapisha Maoni