Jumatatu, Machi 21, 2016

MAFUTA YAIKUTANISHA KENYA NA UGANDA BAADA YA TANZANIA

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anazuru nchini Kenya kesho kukutana na Rais Uhuru Kenyatta kujadili mradi wa bomba la mafuta kati ya nchi hizo mbili.
Ziara ya Museveni inafanyika siku chache tu baada ya Uganda kukubaliana na Tanzania kwamba itajenga mfereji wa kusafirisha mafuta kutoka Uganda hadi Tanzania. 
Wiki jana ofisi ya Rais nchini Tanzania ilitangaza kwamba kampuni ya Total ambayo ina mgao kwenye raslimali ya mafuta nchini Uganda imetenga dola bilioni 4 za kufadhili ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda kuanzia mwezi Agosti.

0 comments:

Chapisha Maoni