Jumamosi, Machi 19, 2016

VITAMIN D NI MUHIMU KWA AFYA YA MATITI

Utafiti wa awali ulithibitisha kuwa ukosefu wa vitamin D utaongeza haratani ya kupata saratani ya matiti. Watafiti wa chuo kikuu cha Stanford cha Marekani wamegundua kuwa ukosefu wa vitamin D pia utaongeza kasi ya ukuaji wa uvimbe wa matiti na kuzifanya seli za saratani zihamie kwa urahisi katika eneo lingine la mwili.
Watafiti walifanya jaribio katiak panya, ambalo waliwalisha panya wa kikundi cha kwanza chakula cha kawaida, na panya wa kikundi cha pili chakula kinachokosa vitamin D. Baada ya muda kadhaa, watafiti wakagundua kuwa kwenye miili ya panya waliokula chakula kinachokosa vitamin D, kasi ya ukuaji wa uvimbe ni haraka kuliko panya waliokula chakula cha kawaida.
Watafiti hao wamesema, ukosefu wa vitamin D unaweza kusababisha seli za uvimbe zisizohama kuhamia sehemu nyignine. Hivyo wameshauri wanawake wafahamu umuhimu wa vitamin D na kula chekula chenye vitamin hiyo.
Lakini watu wana maoni tofauti na idadi ya Vitamin D. Uingereza inawashauri wajawazito, wazee wenye umri zaidi ya miaka 65 na watu wanaokaa chumbani kwa muda mrefu kula vitamin D miligramu 0.01 kila siku. Ulaji wa vitamin D kupita kiasi utaweza kuharibu ini, mufumo wa mishipa ya damu ya moyo.

0 comments:

Chapisha Maoni