Watafiti wa chuo kikuu cha Okayama na chuo kikuu cha Hokkaido wamegundua
kuwa katika pumzi la watu wenye uchafu kwenye ulimi, kiwango cha
acetaldehyde ni cha juu. Acetaldehyde inadhaniwa kuwa kituo kinachoweza
kusababisha saratani ya mdomo na koo, hivyo kusafisha utando wa ulimi
kutasaidia kukinga saratani hizo.
Watafiti hao walichunguza watu 65 wenye afya, na wakagundua kuwa kwa kulinganishwa na watu wenye utando uliofunika theluthi moja ya eneo la ulimi, kiwango cha acetaldehyde katika pumzi la watu wenye utando uliofunika theluthi mbili ya eneo la ulimi ni mara 3.
Utafiti huo pia umeonesha kuwa baada ya kusafisha uchafu wa ulimi, kiwango cha acetaldehyde katika pumzi pia kitapungua.
Watafiti hao wamesema, wataendelea kuchunguza uhusiano kati ya uchafu wa ulimi na saratani.

0 comments:
Chapisha Maoni