Simba aliyetoka katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Nairobi
amemshambulia mzee mmoja katika barabara kuu ya Mombasa Road karibu na
eneo lala City Cabanas.
Afisa wa mawasiliano wa Shirika la Huduma
kwa Wanyamapori (KWS) Bw Paul Udoto amesema kwamba muathiriwa huyo
alikuwa na umri wa miaka 63 na alikimbishwa katika kituo cha matibabu
ya dharura katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na baadaye akapelekwa
katika hospitali kwa matibabu kamili. Simba huyo ameelekezwa ndani
kwenye mbuga.
Maafisa wanaendelea kushika doria kubaini iwapo kuna simba wengine walitoka mbugani.
0 comments:
Chapisha Maoni