Alhamisi, Machi 17, 2016

USIYOYAJUA KUHUSU MADIRISHA YA NDEGE

Madirisha ya ndege ni madogo sana, kwa nini wasanifu wa ndege wasisanifu ndege zenye madirisha makubwa?
Usanifu wa muundo wa ndege ni muhimu sana, na unahitaji kuhakikisha ndege inakuwa nyepesi na imara. Kutoboa sehemu yoyote kwenye ukuta wa ndege kutapunguza uimara wake, na inawabidi wasanifu waweke vipuri vya ziada ili kuhakikisha ndege inaendelea kuwa imara. Hivyo kuweka madirisha mengi makubwa si jambo zuri kwa muundo wa ndege.
Madirisha ya ndege huwa na vioo viwili vya acrylic, ili kuzuia baridi isiingie ndani na pia kupunguza kelele za injini.
Ukiangalia kwa makini madirisha hayo, utaona tundu dogo kwenye kioo cha ndani. Tundu hilo linafanya kazi gani?
Kama tunavyojua, katika anga ya juu shinikizo la hewa ni dogo sana, lakini abiria wanahitaji kukaa katika mazingira yenye shinikizo la kawaida la hewa. Kioo cha nje kinahakikisha shinikizo la hewa ndani ya ndege, na kutokana na tundu hilo dogo, kioo cha ndani hakikabiliana na shinikizo la hewa. Ajali ikitokea, kioo cha nje kitavunjika, kioo cha ndani kitahakikisha usalama wa abiria. Licha ya hayo, tundu hilo pia linasaidia kuondoa mvuke kati ya vioo hivyo viwili ili kuzuia mvuke usigande kwenye kioo cha nje.

0 comments:

Chapisha Maoni