Nchi 8 za Afrika ziko kwenye orodha ya nchi zenye watu wasio na furaha kabisa kwa mwaka 2016
Kwa mujibu wa World Happiness Report ya mwaka huu iliyotolewa jana na chuo kikuu ya Columbia, nchi 10 zilizoorodheshwa kuwa na watu wasio na furaha kabisa duniani ni Madagascar, Tanzania, Libya, Guinea, Rwanda, Benin, Afghanistan, Togo, Syria na Burundi, ambazo zinachukua nafasi 8 kati ya 10. Ripoti ya mwaka huu inatumia vigezo vya furaha kwa kuangalia vigezo zaidi ikiwa ni pamoja na maendeleo endelevu ya kimaumbile na uhifadhi wa mazingira. Gazeti la New York Times linasema, nchi hizo zote zinakabiliwa na umaskini, na baadhi zinakumbwa na vita au maambukizi ya magonjwa, au vyote.
0 comments:
Chapisha Maoni