Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limesema uchumi wa Tanzania unaendelea vizuri, na makadirio ya shirika hilo yanaonyesha kuwa uchumi wa Tanzania kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 7.
Ujumbe wa shirika hilo uliokuwa Tanzania ulifanya mazungumzo na maofisa waandamizi wa serikali ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mawaziri wa fedha, nishati na gavana wa benki kuu, pamoja na wawakilishi wa jumuiya za biashara na wahisani.
IMF pia imepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kupambana na ufisadi.
0 comments:
Chapisha Maoni