Alhamisi, Machi 24, 2016

SHIRIKA LA HALI YA HEWA: JOTO KALI KUENDELEA KUWEPO

Shirika la hali ya hewa la Umoja wa Mataifa (WMO) limesema kuwa, hali ya joto kali itaendelea kuwepo.
Katibu mkuu wa Shirika hilo Petteri Taalas amesema kuwa, hali ya hewa, mwaka jana ilikuwa ya kipekee.
Amesema, "Ulikuwa ni mwaka wenye joto kali zaidi katika historia, na tulikuwa tunavunja rekodi nyingi, na ujumbe muhimu wa pili ambao naweza kuwaambia ni kwamba, tayari tuko karibu sana na kiwango hiki cha ongezeko la nyuzijoto 1.5, na kama ukihesabu miezi michache katika mfulumizo wa muda wako, inaonyesha kuwa tayari tunakaribia hapo"
Wakati huohuo, joto kali limeikumba Kenya, huku joto likifikia zaidi ya nyuzi 40 katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Wimbi hilo la joto ambalo halikutarajiwa limekuwa gumzo nchini humo, na watu wengi wakisema ni mara yao ya kwanza kushuhudia hali ya hewa yenye joto kali, hususan mwezi huu ambao mvua zinatakiwa kuanza kunyesha.

0 comments:

Chapisha Maoni