Alhamisi, Machi 03, 2016

TIMU MAALUMU YA WAKIMBIZI KUSHIRIKI MICHUANO YA OLIMPIKI

Kamati ya kimataifa ya Michezo ya Olimpiki IOC imetangaza kuunda timu ya wachezaji wakimbizi ili kukaribisha michezo ya Olimpiki itakayofanyika huko Rio de Janeiro, Brazil tarehe 5 hadi 21 Agosti mwaka huu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo Bw. Thomas Bach amesema lengo la kuunda timu hiyo ni kutoa ishara ya matumaini kwa wakimbizi duniani. Wachezaji wakimbizi watakuwa na nyumba zao katika kijiji cha Michezo ya Olimpiki kama wachezaji wengine elfu 11 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 200.
Timu hiyo itaundwa na wachezaji watano hadi kumi, ambao watateuliwa na kamati ya utendaji ya IOC kwa mujibu wa uwezo wao wa michezo, hadhi ya ukimbizi iliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa, na uzoefu wao.
Kabla ya hapo, Umoja wa Mataifa ulitoa mwito wa kusimamisha mapambano yote wakati wa michezo ya Olimpiki.

0 comments:

Chapisha Maoni