Alhamisi, Machi 03, 2016

MARUFUKU YA KUWEKA PICHA ZA WATOTO MITANDAONI NCHINI UFARANSA

Wazazi wa Ufaransa wapigwa marufuku kuweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii.
Ufaransa imeweka sheria mpya inayozuia wazazi kuweka picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii bila idhini yao. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kuweka picha ya mtoto kwenye mtandao wa kijamii ni kosa ambalo adhabu yake ni faini ya Euro elfu 45, au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja. Polisi wa Ufaransa wana wasiwasi kuwa kuna uwezekano picha zinazowekwa kwenye mitandao ya kijamii zikatumiwa na wahalifu na kuwaathiri watoto. Na watoto wengine huwa wanataka wazazi wao waheshimu faragha zao, na hawataki picha ziwekwe kwenye social media.

0 comments:

Chapisha Maoni