Jumatano, Machi 02, 2016

TIBA YA JENI YA KUPUNGUZA UZITO YAWEZA KUEPUSHA OSTEOPOROSIS

Njia ya kawaida ya kupunguza uzito inaweza kusababisha osteoporosis, lakini watafiti wa Marekani wamegundua kuwa, tiba ya jeni inaweza kuchochea ubongo kuzalisha homoni maalumu, ambayo inaweza kupunguza uzito na kuepusha osteoporosis.
Watafiti wa chuo kikuu cha Oregon na chuo kikuu cha Florida waliweka jeni maalumu katika ubongo wa panya na kuzalisha homoni maalumu, halafu kuangalia uzito na hali ya mifupa ya panya.
Watafiti wakagundua kuwa uzito wa panya hao ulipungua kwa asilimia 20, lakini hali ya mifupa haikubadilika. Wakati huohuo, mafuta ya tumboni ya panya yalipungua kidhahiri, ambayo yanahusiana na suala la kiafya.
Watafiti walisema, njia ya kawaida ya kubana ulaji wa chakula, itapunguza uzito wa mifupa. Hivyo tiba ya jeni ya kupunguza uzito haitaathiri uzito wa mifupa. 
Lakini watafiti waliongeza kuwa, tiba hiyo bado inahitaji majaribio mengi zaidi, ili kuthibitisha tiba hiyo haidhuru afya.

0 comments:

Chapisha Maoni