Jumatano, Machi 02, 2016

KWA NINI MILANGO NA MADIRISHA YA NDEGE HAYAWEZI KUFUNGULIWA OVYO?

Kwenye ndege iliyoahirishwa kuruka, abiria mmoja alifungua mlango ili apate hewa nzuri, lakini baadaye alilazimishwa kushuka na kutozwa faini. Kitendo chake si kama tu kilikwenda kinyume na kanuni za shirika la ndege, bali kingeweza kusababisha ajali kubwa.
Mazingira ndani ya nege yanabadilika baada ya ndege kuruka. Ikifika uswa wa mita 8000 kutoka usawa wa bahari, shinikizo la hewa nje ya ndege linapungua kwa zaidi ya nusu, na baridi inakuwa kali hadi nyuzi 50 sentigredi chini ya sifuri. Abiria akifungua mlango katika usawa huo, watu wote kwenye ndege watakuwa hatarinu au kufa. Sababu ni kwamba bongo za binadamu haziwezi kupata oxygen ya kutosha kutoka kwenye mazingira kama hayo, na watazirai mara moja. Shinikizo la hewa likipungua ghafla, hewa iliyoko ndani ya tumbo litapanuka mara moja na kuleta madhara kwa binadamu.
Aidha, mlango ukifunguliwa wakati ndege inaruka, huenda abiria wakaanguka kutoka ndege kutokana na upepo mkubwa.

0 comments:

Chapisha Maoni