Watafiti wa Marekani wamegundua kuwa kupunguza ulaji wa sukari tu kutaweza kuponesha maradhi mengi ya umetaboli ya vijani likiwemo shinikizo kubwa la damu.
Watafiti wa chuo kikuu cha California na chuo kikuu cha Touro wamesema, katika hali ya kutopunguza idadi ya chakula na kutopunguza uzito, kupunguza ulaji wa sukari kunaweza kuponesha lehemu ya juu na shinikizo kubwa la damu la vijana.
Utafiti huo umechunguza watoto na vijana 43 kutoka miaka 9 hadi 18, ambao wote wamepata maradhi ya umetaboli. Watafiti waliwaandalia chakula kwa siku 9, ambacho kiwango cha sukari kilipungua kutoka asilimia 28 hadi 10.
Watafiti wamegundua kuwa baada ya siku tisa, hali ya afya ya vijana hao imeboreka. Watafiti wamesema, ulaji wa sukari nyingi unaleta athari mbaya kwa mwili, sukari hizo zinabadilishwa kuwa mafuta katika ini, kusababisha kinga ya insulini na kuongeza hatari ya ugonjwa wa kisukari, moyo, na ini.
0 comments:
Chapisha Maoni