Jumatano, Machi 02, 2016

KABURI LINGINE LA HALAIKI LAFUKULIWA BURUNDI

Maafisa wa usalama nchini Burundi wamefukua kaburi la halaiki katika kitongoji cha Mutakura, viungani mwa mji wa Bujumbura na kupata miili 30.
Miili hiyo inaaminika kuwa ya watu waliounga mkono rais Pierre Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu, Freddy Mbonimpa, meya wa manispaa ya Bujumbura aliambia waandishi wa habari. "Waliuawa na miili yao ikazikwa hapa ikiwa imewekwa kwa mifuko ya plastiki," alisema Mbonimpa. "Wengi wao ni vijana wa Imbonerakure," alisema. Imbonerakure ni kundi la vijana wanaounga mkono uongozi wa rais Pierre Nkurunziza.
Kitongoji cha Mutakura kinaaminika kuwa mojawapo ya makaazi ya wapiganaji mjini Bujumbura. Burundi imeshuhudia michafuko tangu mwezi Aprili mwaka uliopita rais Nkurunziza alipotangaza kuwania muhula wa tatu. Nkurunziza hatimaye aliwania na kushinda uchaguzi huo mwezi wa Julai mwaka jana.

0 comments:

Chapisha Maoni