Watafiti wa chuo kikuu cha Osaka wamegundua kuwa kuacha uvutaji wa sigara kunaboresha ugonjwa wa ger.
Ger ni ugonjwa ambao vitu vilivyomo tumboni vinarudi katika umio na kusababisha hisia za kutapika. Kama ugonjwa huo unazidi kuwa mbaya, utasababisha kutokwa damu kwenye tumbo hata saratani. Imefahamika uvutaji wa sigara ni moja ya vyanzo vya kusababisha ugonjwa huo.
Watafiti walifuatilia hali ya wagonjwa 73 wa ger, ambao walitumia miezi mitatu kuacha uvutaji wa sigara. Katika mwaka mmoja uliofuata, kati ya watu 51 wasiorejesha tabia ya kuvuta sigara, hali ya ugonjwa ya watu 22 iliboreshwa, ambayo ilichukua asilimia 43. Lakini kati ya watu wengine 22 walioendelea kuvuta sigara, watu wanne tu walipata nafuu.
0 comments:
Chapisha Maoni