Mji mkuu wa Mauritius, Port Louis, umetajwa kama mji bora zaidi kuishi katika bara la Afrika. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kampuni ya utafiti ya Mercer.
Ripoti hiyo ambayo ilitolewa Jumapili jijini London, Uingereza iliweka Port Louis katika nafasi ya 83 kote duniani mbele ya miji mikubwa ya Afrika Kusini kama Durban ambao uliorodheshwa katika nafasi ya 85, Cape Town (92) na Johannesburg (95).
Miji mengine ya bara la Afrika ambayo yalifanya vyema kulingana na orodha hiyo ni Windhoek ya Namibia ukichukua nafasi ya 131 na Gaborone, Botswana ukichukua nafasi ya 142 kote duniani.
Baadhi ya maswala yaliyoangaziwa kwenye utafiti huo ni pamoja na hali ya usalama, mazingira ya kisiasa na kijamii, hali ya kiuchumi, vifaa vya matibabu na afya, mfumo wa elimu, huduma za usafiri wa umma, miundombinu ya miji, burudani na makazi.
Mji wa Vienna nchini Austria ulitajwa kama mji bora zaidi kote duniani kuishi ukifuatwa na Zurich nchini Switzerland, Auckaland, Munich na Vancouver.
0 comments:
Chapisha Maoni