Jumatano, Machi 02, 2016

BARA BARA YA KUTOKA TANZANIA KUPITIA ARUSHA-HOLILI-TAVETA-VOI NCHINI KENYA

Marais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenziye John Magufuli wa Tanzania wanatarajiwa kuzindua mradi wa ujenzi wa bara bara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi ambayo inaunganisha nchi hizo mbili siku ya Alhamisi hii wiki.
Tayari hafla maalum imetengwa ya kuzindua mradi huo wakati wa kongamano la marais wa shirikisho la Afrika mashariki litakaloanza kesho (Mechi 2) mjini Arusha, Tanzania. Ujenzi wa bara bara hiyo unatarajiwa kuimarisha usafirishaji wa bidhaa na watu kati ya nchi hizo jirani. Utakapokamilika, bara bara hiyo itaunganisha bandari ya Mombasa nchini Kenya na Tanzania kaskazini.

0 comments:

Chapisha Maoni